WANYAMA WATANO WAKUBWA MBUGANI

FAHAMU UNDANI WA WANYAMA WAKUBWA WATANO PORINI



Bara la Afrika ndio bara pekee duniani liloweza kubarikiwa kuwa na wanyama wa tano wakubwa wa porini.
Wanyama hawa hawakuchanguliwa kwakuangalia ukubwa wa miili yao ila nikutokana ugumu wa kuwindwa na pia ndio wanyama hatari na wenye hasira kali kuliko wote. Wanyama hao ni pamoja na Tembo, Faru, Nyati , Simba na Chui.

Nchi pekee barani Afrika ambazo wanyama hawa wakubwa wa tano hupatikana ni pamoja na nchi ya Tanzania, Botswana, Zambia, Uganda, Namibia, Ethiopia, Afrika ya Kusini, Kenya, Zimbambwe, Kongo, na Malawi.

Tembo

Tembo ndio mamalia mkubwa kuliko wote dunia, huwa na ngozi isiyona na vinyoleo, meno marefu na yaliotokeza kwe nje. Kuna spishi mbili za tembo moja ni tembo wapatikanao katika misitu na pia tembo wapatikanao katika vichaka. Tembo huishi katika familia ya makundi isiyo pungua tembo mia moja huku kiongozi wa familia akiwa ni tembo jike.

Faru
Faru ni mamalia wa pili kwa ukubwa baada ya tembo, huku kukiwa na spishi mbili za faru wapatikanao barani Afrika ambazo ni faru mweupe na faru mweusi. Utofauti ya faru hawa ni kwenye namna ya midomo yao ilivyo kaa na sio rangi kama wengi wananyodhani.

Kwa bahati mbaya hivi sasa wanyama hao wamekuwa wakipungua kutokana na ongezeko la ujangili uliokithiri barani Afrika. Pembe ya faru inasadikika kutumika kama tiba ya magongwa mbalimbali hasa bara la Asia.

Mwaka 2012 pembe ya faru ilikuwa ikiuzwa dola 60,000 kwa kilo. Tukiweza kuzuia ujangili faru wataweza kuishi hadi miaka 30-50.

Nyati


Nyati dume hukuwa na kufika futi 4-6 na kilo 700, nyati amehesabika kupoteza maisha ya watu wengi kuzidi wanyama wengine wa porini. Ni mnyama mwenye hasira kali sana na pia ni hatari sana.

Mnyama huyu humuwia vigumu hata samba wakati wa kuwinda na humbidi samba kupata msaada kutoka kwa wenzake ndio waweze kumuangusha nyati mmoja.

Simba


Simba ndio paka mkumbwa kati ya wapatikano bara la Afrika. Dume huwa na manyoya kuanzia kwenye mabega yake nakuelekea kwenye kichwa chake. Simba huweza kuishi hadi miaka kumi na nane akiwa porini, lakini wengi wao hupoteza maisha kutokana na kupingana kati ya wenyewe kwa wenyewe.

Simba jike ataishi kwenye familia yake huku dume atatolewa katika familia akiwa na miaka 2-4 na kuanza kwenda kujitengemea.

Chui


Ni moja kati ya paka wakubwa watano wapatikanao porini ila imekuwa vigumu sana kumuona chui hata ukiwa porini nikutokana na mazingira ambayo amekuwa akishi. Chui upendelea kuishi juu ya miti na kutumia mazingira hayo kama njia yake ya kujilinda.

Chui ni nusu ya uzito wa simba ila anauwezo wa kubeba mnyama na kupanda nae juu ya mti.


PORINI LEO IMEANDALIWA NA;
WILLIAM WESTON KATOLE ( KIDAYO )

FB @kidayoo_tz
Instagram @kidayoo_tz
Contact  +255 659 214 411
Email: kidayotv@gmail.com


Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA YA MAISHA YA MSANII WA BONGO FLEVA HARMONIZE.

MSANII MPYA WA HARMONIZE ATAMBULISHWA LEO, KONDE MUSIC WORLDWIDE

JE WAJUA HII KISUKARI HUSABABISHA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME.