MSANII MPYA WA HARMONIZE ATAMBULISHWA LEO, KONDE MUSIC WORLDWIDE

Harmonize amsainisha Ibraah kama msanii wa kwanza Konde Gang


Msanii chipukizi, Ibraah Tz ameandika historia kama msanii wa kwanza kusajiliwa katika record Label ya Muziki ya Konde Music Worldwide, iliyo chini ya msanii Harmonize.
kupitia mitandao yake ya kijamii, Konde Boy IG amethibitisha kuwa Ibraah sasa ni msanii rasmi wa Konde Gang.
Harmonize alishukuru uongozi wa Konde Gang kwa kuahidi kuendelea kujinyima ili Ibraah aweze kutimiza ndoto zake.


Konde Boy pia alimmiminia Ibraah sifa tele huku akihakikishia mashabiki wake kuwa, siku yenye atastaafu mambo ya usanii, ana Imani msanii huyo mpya ataendeleza kazi yake.
“Naweza sema bila shaka hata ikitokea siku siimbi muziki tena naamini Ibraah ni mtu ambaye anaweza fanya kila ninacho fanya .” Alisema Harmonize.
Msanii huyo wa zamani wa Wasafi Classic, alitangaza usajili wa Ibraah siku moja tu baada ya Diamond kutangaza kumsajili zuChu, ambaye ni mwanawe Khadija Kopa.
Hivi basi yatakuwa mashindano kati ya label hizi mbili na wasanii hao wapya kuonesha ubabe wao.
 
Kupitia ukurasa wake wa Instagram Harmonize ameandika kuwa anaamini ikitokea ameacha kuimba basi Ibraah TZ ndiye Msanii anayeweza kufanya yote ambayo yeye anaweza kufanya.


'Nafsi Inaniambia Mungu Anaetoa Na Kubariki Vipaji Ndie Mungu Anaegawa Upendo Katika Nyoyo Za Waja Wake Safii Na Nyeupe....!!! Binafsi Natambua Uchanga Wa Kampuni Inayonisimamia Pia Natambua Changamoto Tulizotoka Kupitia Punde..!!! Kifedha Naamini Kinachotufanya Mpaka Tuwe Hapa Leo Ni Dua Zenu Pamoja Na Upendo Ambao Nibaraka Toka Kwa Mungu Kama Unavyotambua Mambo Haya Ya Kusimamia Msanii Ama Wasanii Yanahitaji Uwekezaji Mkubwa Sana...!!! Richa Ya Kujinyima Kujichanga Changa Tunako Endelea Nako Lakini Haijawa Sababu Ya Kuruhusu





MSANII WA HARMONIZE KUPITIA RECORD LABEL YA KONDE GANG AMETAMBULISHA NYIMBO YAKE MPYA. VIDEO NA AUDIO - NIMEKUBALI.


FOLLOW HIM INSTAGRAM, FACEBOOK, YOUTUBE NA TWITTER

 
 For more info follow instagram Afisa Habari wa Harmonize @msemaji_wa_harmonize_tz

Comments

Post a Comment

Popular posts from this blog

HISTORIA YA MAISHA YA MSANII WA BONGO FLEVA HARMONIZE.

JE WAJUA HII KISUKARI HUSABABISHA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME.